Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Mohamedi Mnemwa amepewa rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha mifupa MOI kufuatia kipimo cha CT Scan kuonyesha damu yake imevilia kwenye ubongo.
Mnemwa ambaye mchana wa leo amefanyiwa kipimo hicho katika hospitali ya rufaa mkoa wa Temeke hali iliyolazimu kuandikiwa rufaa ya kupelekwa Muhimbili kufuatia baada ya pambano lake la Januari 24, 2025 na kuzimia baada ya kupigwa kwa 'K.O' ya raundi ya tatu dhidi ya bondia Ally Issa Sewe katika pambano la raundi nne mbalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Mrina uliopo TipTop, Manzese jijini Dar es Salaam.
Mnemwa amepelekwa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kufanyiwa kipimo hicho ambacho kimegundua tatizo la kuganda kwa damu kwenye ubongo.
Daktari wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBRC Dk. Hadija Hamisi amesema kuwa bondia huyo tayari amefanyiwa vipimo na amegundulika ana madhara mwilini mwake.
"Mgonjwa ameshafanyiwa kipimo cha CT Scan na amegundulika kuwa damu imevilia kwenye ubongo, anapelekwa Moi, Muhimbili kwa ajili ya kupata vipimo zaidi na Moi watatupa majibu zaidi," amesema Dk. Hadija.
Post a Comment