*******
BENKI ya kibiashara
nchini KCB imesema itaendelea kudhamini sekta ya michezo ili kukuza vipaji vya
michezo.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa KCB Lugalo new Year Competition 2025,Mkuu wa idara ya Masoko,
Mawasiliano na Uhusiano wa KCB Bank Tanzania, Christina Manyenye amesema
“Mbali na Biashara ya
Benk,pia tunajikita kwenye sekta za kijamii ikiwemo michezo ili kuweza kukuza
vipaji kwa Watanzania”Amesema Manyenye.
Manyenye amesema
katika kuhakikisha hilo wameendelea kudhamini mchezo wa Gofu nchini.
“Mwaka jana
tuliwapeleka timu ya gofu nchini Kenya,na mwaka huu tutawapeleka tena Kenya na
tunataka wakienda kule waje na ushindi,”Amesema Manyenye.
Amesema nia ya Benki
hiyo kudhamini mchezo huo ni kuhakikisha kwenye mchezo wa Gofu unasonga mbele.
Aidha,Mkuu huyo wa
masoko ametumia nafasi hiyo kuwahimiza watanzania kutumia huduma za kidigitali
za Benki hiyo kwa kufanya miamala mbalimbali.
“KCB Bank tupo
kidigitali tunawataka wananchi wafanye miamala yao kutumia simu haina haja ya
kwenda Benk unatumia simu yako kufanya miamala,na sisi tunamjwakala nchi
nzima,lengo letu tunawapa wigo wateja wetu kutumia kidigitali”Amesema
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Klabu ya Gofu Lugalo (TPDF Lugalo Golf Club,Brigedia Jenerali
Mstaafu, Michael Luwongo,ameishukuru Benk ya KCB kwa udhamini wake na amesema
kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na mashindano mengi.
Mwenyekiti pia
alishiriki mipango ya kuboresha miundombinu ili kuhakikisha uendelevu wa klabu
hiyo. “Tunashukuru kwa mvua tulizopata mwaka jana, zilizosaidia kutunza viwanja
vyetu. Hata hivyo, tunafanya kazi ya kuchimba kisima ili kupata chanzo cha maji
ya uhakika na kujenga jukwaa lenye taa za mionzi. Hii itawawezesha wanachama
wetu kufanya mazoezi hata usiku, na kuondoa vizuizi vinavyosababishwa na giza
la mchana,” alisema.
Mbali na kuwapongeza
washiriki wote katika mashindano, KCB Bank ilitangaza mipango ya kuandaa semina
endelevu za kukuza mchezo wa gofu nchini na kimataifa. Mpango huu unalenga
kukuza talanta, kuboresha ujuzi, na kupanua wigo wa mchezo katika kanda hiyo.
Mashindano ya Gofu ya
Mwaka Mpya yalionyesha umuhimu wa ushirikiano kati ya mashirika ya biashara
kama KCB Bank na taasisi za michezo kama Lugalo Golf Club. Kwa pamoja, wanakuza
upendo wa mchezo lakini pia wanaunda fursa za maendeleo binafsi na kitaaluma
katika sekta ya michezo ya Tanzania.
Post a Comment