Watu 16 wamekufa kutokana na moto mkubwa wa nyika, unaoendelea
kuteketeza eneo la mji wa Los Angeles katika jimbo la California nchini
Marekani.
Watu 11
walikufa katika moto wa Eaton karibu na Pasedena na wengine watano wamefariki
katika moto mwingine unaowaka kwenye wilaya ya Pacific Palisades.
Idara ya zimamoto
inakadiria kwamba zaidi ya nyumba 5,300 zimeteketea kwa moto katika kitongoji
cha Pacific Palisades tangu siku ya Jumanne huku majengo zaidi ya 7,000
yakihofiwa kuchomeka katika eneo la Eaton.
Mkuu wa idara ya
zimamoto Antony Marrone ameonya kwamba kitisho cha moto kinasalia kuwa juu
kwasababu ya upepo mkali, hali ya hewa na uoto mkavu.
Naye Gavana wa
California Gavin Newsom, ameeleza kwamba vikosi vya zima moto kutoka Mexico
vimewasili mjini humo kusaidiana na maafisa takribani 14,000 wanaopambana
kuudhibiti moto huo.
Cc DWkiswahili
Post a Comment