Klabu ya Simba imefuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Bravos do Marquis ya Angola katika Uwanja wa Estádio Da Tundavala, kwenye mchezo wa raundi ya tano ya Kundi A.
Kwa mujibu wa kanuni za CAF, Simba SC imefaidika na matokeo ya head-to-head, baada ya kuifunga Bravos kwenye mechi ya awali na kutoka sare kwenye marudiano. Hii inamaanisha Bravos tayari imeondolewa kwenye mashindano hata Simba ikipoteza mchezo wake wa mwisho.
Post a Comment