****
Waziri wa fedha, Dkt Mwigulu Nchemba, amezielekeza taasi za fedha Nchini kujiorodhesha kwenye soko la Hisa la Dar es salaam ili kufanya uwekezaji wenye tija kwa maslahi mapana ya Taifa.
Waziri Dkt Mwigulu maelekezo hayo Jijini Dar es salaam wakati akizindua hati fungani ya benki ya Azania iliyopewa jina la Bondi Yangu na kuorodheshwa rasmi katika soko la Hisa la Dar es salaam ambapo ametumia nafasi hiyo kuzitaka Tasisi nyingine kuiga mfano wa benki hiyo.
Aidha,amesema Serikali kupitia wizara hiyo imekuwa ikihamasisha uwekezaji wenye tija huku kuorodheshwa taasisi hizo kwenye soko hilo Hisa itasaidia kusukuma mbele uchumi wa Tanzania.
Hata Hivyo,Dkt Mwigulu ameipongeza Benki ya Azania kwa hatua yake kuorodheshwa kwenye soko la hisa kwa kusema hatua hiyo inakuza uchumi na inaendana na maono ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Dkt Esther Mang’enya amesema mauzo ya hatifungani hiyo imevuka lengo la asilimia miambili na kumi.
Peter Nalitolela ni Afisa Mtendaji Mkuu soko la Hisa la Dar es salaam –DSE amesema uwekezaji katika soko hilo imeendelea kuongezeka ambapo hadi kufikia januari 23 mwaka huu zaidi ya laki 6.
Hatifungani ya Benki ya Azania benki ilianza mwezi Novemba na kufungwa mwezi Disemba mwaka jana pamoja na kupewa idhini kutoka mamlaka ya masoko ya mitaji kuongeza kiwango ya kuchukua zaidi ya fedha iliyopatikana.
Post a Comment