YANGA YAIFUNZA MAZEMBE BOLI,YAICHAPA (3-1)

..........

NA MUSSA KHALID 

Timu ya Yanga SC ya Tanzania imeibuka na ushindi wa magoli matatu kwa Moja (3-1) dhidi ya Timu ya TP Mazembe kutoka DRC katika mchezo wa ligi ya Klabu Bingwa Afrika ambao umemalizika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa ni wakasi kwa timu zote kuonyesha ufundi uwanjani TP Mazembe ndio Ilikuwa ya kwanza kupata bao na Kisha Yanga SC ikasawazisha na kufanya Kipindi cha kwanza kumalizika Kwa goli (1-1).

Hata hivyo timu hizo baada ya kurejea Kipindi cha pili Yanga SC ndio imeonekana shujaa baada ya kufunga magoli mawili na hivyo kufanya mchezo huo kumalizika Kwa Jumla ya Magoli (3-1)

Katika mchezo huo magoli ya Yanga yamefungwa na Clement Mzize aliyefunga mawili na lingine likifungwa na Stephan Azizi Ki na hivyo kufanya timu hiyo kufikisha alama 4 katika michezo yake iliyocheza.

0/Post a Comment/Comments