Zanzibar,
Februari, 2025 – Airtel Afrika imeingia kwenye
ushirikiano na wadau wa muziki kukuza vipaji vya muziki Afrika kupitia
teknolojia ya mawasiliano ya intaneti ya kasi ili kuhakikisha wasanii wanafikia
ndoto zao.
Kampuni hiyo
ilidhihirisha dhamira hiyo kwa kushirikiana na jukwaa la Trace Awards and
Summit 2025 iliyofanyika The Mora visiwani Zanzibar kuanzia Februari 24 hadi
26.
Jukwaa la Trace
Awards2025 lilizinduliwa rasmi na Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi ambae
aliahidi kuwa serikali iko tayari kutoa mchango kwa sekta ya muziki kwa
kuwaunga mkono wasanii na kuweka mazingira rafiki kwa ajili ya ukuaji wa sekta
hiyo.
“Tunaamini katika nguvu
ya sekta ya burudani katika kuchochea mabadiliko. Muziki ni nyenzo muhimu
katika uwezeshaji, kukuza utalii, kuleta maendeleo ya kiuchumi na maendeleo ya
kijamii. Pia nachukua nafasi hii kuwapongeza na kuwashukuru wadau wote
waliofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha tukio hili linafanyika kwa
mafanikio,” alisema Mwinyi.
Akizungumza kuhusu ushiriki
wa Airtel Africa kwenye tuzo hizo, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania,
Timea Chogo alibainisha kuwa hatua hiyo inatokana na dhamira ya Airtel
kuhakikisha inatoa fursa kwa kila mtu kuweza kufikia ndoto zake.
“Kufanyika kwa tamasha
pamoja na utoaji tuzo za TraceAward2025 visiwani Zanzibar kunatengeneza fursa
za kiuchumi na kuendelea kuwafungulia dirisha wasanii wetu kimataifa. Ni jambo
lakufursahisha mwaka huu tunafanya tamasha Tanzania tukiwa na wasanii tisa
wanaowania tuzo hizi. Hii ni sababu tosha kwa Airtel kuweza kushiriki kuungana
na wasanii hao kupitia muunganiko wa kibunifu na mtandao ili waweze kuusambaza
muziki wao ndani na nje ya Tanzania,” alisema Chogo.
Kwa upande wake, Balozi
wa Airtel Tanzania, Diamond Platnumz alisema; Trace awards inajumuisha watu
wote kutoka Afrika na nje ya Afrika wanakuja hapa.
“Trace awards imeleta
watu wote kutoka Afrika na nje ya Afrika kukutana hapa. Uwepo wa Airtel
unasaidia watu waliokuja kwenye tuzo hizi waweze kuunganishwa na data na kupata
huduma zingine zitakazowasaidia kuwasiliana na ndugu na jamaa na kuwawezesha
kufanya biashara na hali kadhalika kushare maudhui yao na wasanii wengine.”,”
alisema Diamond Platnumz.
END.
Post a Comment