BABA MZAZI WA WAZIRI MCHENGERWA AFARIKI

...............

Baba mzazi wa Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohammed Mchengerwa, Alhaj Omary Mchengerwa  amefariki dunia akishiriki Ibada ya Umrah.

Alhaj Omary Mchengerwa amefikwa na msiba alfajiri ya leo Jumatatu Februari 24, 2025 akiwa katika Ibada hiyo Umrah Makkah. 

Taarifa ya familia imesema kuwa Alhaj Omary atazikwa leo  mchana Makkah. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, dua maalumu ya kumuombea marehemu itafanyika leo jioni nyumbani kwa mtoto wake, waziri Mchengerwa Masaki Jijini Dar es Salaam na kesho dua maalumu itafanyika nyumbani kwa marehemu Yombo.

Inna lillahi wa Inna Illahi rajiun

0/Post a Comment/Comments