*****
Aliyekuwa baba wa Taifa la Namibia, Rais mstaafu Dk Sam Mwakangale amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa leo asubuhi na Rais wa Namibia, Dk Nangolo Mbumba kwa wananchi wa Taifa hilo imelezea kuwa Dk Nujoma amefikwa na umauti baada ya kuwa hospitalini kwa takribani wiki tatu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk Nujoma aliyepigania uhuru wa Taifa hilo, ameaga dunia jana saa 5.46 usiku jijini Windhoek, Namibia alipokuwa amelazwa kwa wiki tatu.
Rais Nujoma aliyekuwa na uhusiano mzuri na Watanzania pamoja na wapigania uhuru wa nchi hiyo walipigana na hatimaye Namibia ilipata uhuru wake Machi 21,1990.
Kufuatia kifo hiko, Rais Mbumba ametangaza kipindi cha maombelezo wakati serikali ikiendelea na taratibu za mazishi ya kiongozi huyo.
Post a Comment