Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kufunga kwa muda barabara nne zinazotumika kuingia katikati ya Jiji, ili kutoa nafasi kwa ugeni wa wakuu wa nchi wanaotarajiwa kukutana kesho, Februari 8, 2025, Jumamosi.
Ugeni huo ni wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo Rais Samia Suluhu Hassan ndiye mwenyeji.
Mkutano huo utajadili mgogoro unaoendelea Mashariki mwa DR Congo kati ya majeshi ya Serikali na vikosi vya M23.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Februari 7, 2025, barabara zitakazofungwa ni Barabara ya Nyerere, kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuelekea katikati ya Jiji.
Pia, Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli zitafungwa kuanzia taa za Gerezani hadi Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency na Ikulu.
Post a Comment