BIHARAMULO WAMPONGEZA DED KUVUKA MALENGO UKUSANYAJI MAPATO


 Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo wakiwa kwenye kikao chao.

****

Na Daniel Limbe, Biharamulo

MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wamempongeza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa ukusanyaji mzuri wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo hali iliyosaidia kupunguza adha katika miradi ya jamii.

Ikumbukwe kuwa halmashauri hiyo ilikusudia kukusanya na kutumia kiasi Cha shilingi 41,077,149,000 katika mpango wa bajeti ya mwaka 2023/24,lakini ilifanikiwa kukusanya na kutumia zaidi ya shilingi bilioni 45,562,406,334 sawa na aslimia 111.

Hayo yameelezwa leo kwenye kikao Cha Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichoketi kupitia utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2023/24 kwa lengo la kujitathimini na kuboresha zaidi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Leo Rushahu,amesema ushirikiano mzuri kati ya watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo umesaidia sana katika ukusanyaji wa mapato ya ndani hali iliyosaidia kupunguza changamoto zilizokuwepo awali.

"Siri kubwa ya kutatua changamoto za wananchi wetu ni kuhakikisha madiwani tunasimamia vizuri mapato ya ndani, hatua hii ndiyo umesaidia kupunguza adha za kukwama kwa miradi ya wananchi wetu,tumpongeze sana mkurugenzi wetu kwa kazi kubwa ya kukusanya na kutumia vyema fedha za umma"amesema Rushahu.

Baadhi ya miradi iliyotekelezwa ni pamoja na nyumba za walimu,ujenzi wa vyumba vya madarasa 57, matundu ya vyoo 112, pamoja na maabara 4 za sayansi.

Mbali na hayo, jumla ya shilingi 203,790,307.51 kilikusanywa kwa lengo la kuwanufaisha wanalengwa wa mikopo ya aslimia 10 ikiwa ni wanawake,vijana na wenye ulemavu,sambamba na hilo jumla ya sh. 138,890,851 zilirejeshwa kutoka kwa vikundi 107.

Kadhalika Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Innocent Mkandara,amewashukuru adiwani kwa usimamizi mzuri wa mapato huku akiwasihi kuongeza jitihada za kudhibiti utoroshwaji wa mapato ya ndani kwenye kata zao.



0/Post a Comment/Comments