Wastaafu Saba (7) wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhudhuria Sherehe ya
kufunga Mwaka iliyoambatana na Tafrija fupi ya kuwaaga wastaafu hao, Ijumaa ya
Tarehe 7 Februari 2025, Nje ya Jengo la Ofisi za COSTECH Iilopo Sayansi- Kijitonyama
– Jijini Dar es salaam.
Faisal
Abdul Jalil
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wamefanya Sherehe ya kufungua Mwaka iliyoambatana na Tafrija fupi ya kuwaaga Watumishi Wastaafu Saba (7) ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango na upendo wao waliouonesha wakihudumu nafasi nafasi mbalimbali za utumishi wa Umma pamoja na Tume hiyo. Ijumaa tarehe 7 Februari 2025, Ofisi za Tume hiyo zilizopo, Sayansi – Kijitonyama – Jijini Dar es salaam.
Akizungumza kupitia Tafrija hiyo, *Kaimu Mkurugenzi Mkuu* , ambaye ni *Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji Tafiti (DRCP)* , Dkt. Zabron K. Bugwesa amewatakia kila la kheri Watumishi Wastaafu hao pamoja na heri ya Maisha Mema kustaafu na kuwapongeza kwa kuitumikia Tume hiyo kwa uamininifu na uadilifu mkubwa.
“ kwa Niaba ya Watumishi Wenzangu
tunawatakia maisha mema Watumishi Wastaafu wetu, tutaendelea kuyaenzi yale mema
na mazuri mliyotuachia, kuendeleza mshikamano na umoja wetu mpaka
tutakapostaafu kwa mujibu wa sheria katika utumishi wa Umma.” alisema Dr. Bugwesa.
Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi (DCS) , Ndg. Imanuel I Mgonja aliwapongeza Watumishi Wastaafu hao na kuwaasa watumishi wa COSTECH kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano , weledi na Uadilifu kwa kuzingatia maadaili ya Utumishi wa Umma. Watumishi Wastaafu hao wakiongozwa na Mkurugenzi Mstaafu wa Huduma za Taasisi Ndg. Shaabani Msangi Husein , Meneja Mipango na Ufuatiliaji Bi. Anna Godwin Ngoo, Mwandishi Mwendesha Ofisi, _Bi. Halima Mohamed Shekimweri, Afisa Mkutubi Mkuu Bi. Justina Shauri_, Mtunza Kumbukumbu, Bi. Arafa Jamadi Mtemba, Afisa Tawala Mkuu Bi. Louise Mary Mdachi pamoja na Mhasibu mstaafu, Ndg. Boniface George Choma_. Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Watumishi Wastaafu walioagwa, Ndg. Shabaani aliwaasa watumishi kufanya kazi kwa ufanisi na kuwa wabunifu.
“Watumishi wa COSTECH pamoja na wanasayansi wetu Tume inawategemea kuhakikisha mnafanya kazi kwa bidii na maarifa kuweza kuiongezea Tume vyanzo vya mapato , kazini ni sehemu nzuri ya kufanya kazi kwa upendo , bidii ,uaminifu, uadilifu, weledi na kujiendeleza kielimu ni vitu vya kuvizingatia sana katika kuimarisha utendaji kazi wenu.” allsema Bw. Shabani.
Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa*, na Meneja wa TEHAMA , Ndg. Daudi Mboma amewapongeza Watumishi Wastaafu hao na kuwataka kudumisha ushirikiano waliokuwa nao kwenye jamii wanayoishi nayo.Kwa upande wake, Meneja Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Vumilia Sailen alisema Tume inatambua mchango mkubwa wa Watumishi Wastaafu hao na hivyo imeamua kugawa Tuzo Maalum kama sehemu ya kuenzi uhudumu wao katika Idara na Vitengo tofauti za Tume hiyo.
Akihitimisha kwa Niaba ya Watumishi ,
Menejimenti na Chama Cha Wafanyakazi cha RAAWU, Bi. Aysha Mgaya aliwapongeza
Watumishi Wastaafu hao kwa kipindi walichohudumu, Mwenyekiti wa Mfuko wa Wafanyakazi wa CSSF, Bi.
Bestina Daniel pamoja na Meneja toka
Kurugenzi ya DRCP, Bi. Hilda Mushi kwa pamoja waliahidi kuendeleza
mazuri yaliyofanywa na Watumishi Wastaafu hao mara baada ya kuahirishwa kwa
Sherehe hiyo iliyofanyika Ofisi za COSTECH zilizopo , Sayansi- Kijitonyama,
Jijini Dar es salaam.
Post a Comment