DK FIMBO AKAGUA UJENZI OFISI ZA MAKAO MAKUU TMDA

*******

Na Tausi Mbowe

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzana (TMDA), Dk Adam Fimbo amekagua maendeleo ya upanuzi wa ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka jijini Dododoma. 

Dk Fimbo amefanya ukaguzi huo katika ziara yake leo  aliyoifanya Jumanne, Februari 11, 2025.

Pamoja na mambo mengine ziara hiyo imelenga kutathimini hatua za ujenzi na kuhakiisha kuwa mradi unaendana na muda na viwango vya ubora. 

Akizungumza katika ziara hiyo, Dk Fimbo alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo na kumtaka mkandarasi kumaliza kwa wakati kulingana na mkataba uliowekwa baina ya pande zote.




0/Post a Comment/Comments