Tausi Mbowe, Dar
Pamoja na jukumu la kusimamia Dawa, Vifaa Tiba na Vitendanishi Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), inawajibika pia kutoa elimu kwa wanafunzi shule na vyuo vinavyotoa elimu ya Afya.
Miongoni mwa wanavyuo hao ni pamoja na Chuo cha Afya Muhimbili.
Vingine ni Chuo cha Afya cha Paradigms College lilichopo jijini Dar es Salaam pamoja na vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Hivi karibuni Mammala hiyo imetoa mafunzo kwa kwa vitendo yanayohusu masuala mbalimbali ya afya.
Wanafunzi hao walipata mafunzo hayo mwishoni mwa mwezi Januari 2025 katika ofisi za Mamlaka hiyo Kanda ya Mashariki zilizopo jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine wanafunzi hao wamejifunza kwa vitendo mambo mbalimbali ya Dawa, Vifaa na Vitendanishi.
Sambamba na mafunzo hayo wanafunzi hao walipata fursa ya kutembelea maabara za kisasa zilizopo katika ofisini hiyo.
Post a Comment