*****
Na Ester Maile, Dodoma
Wakurugenzi wa halmashauri za Dodoma wametakiwa kujipanga kuboresha mwonekano wa jiji la Dodoma hasa katika eneo la Stesheni ya Treni ya Mwendokasi SGR.
Haya yamesemwa na Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ukarabati wa soko kuu la majengo pamoja na ujenzi wa stand za daladala na vivuko vya ntyuka ,chadulu na mailimbili .
Mchengerwa amewataka wakandarasi wa miradi ya nyuma pamoja na utengenezaji wa barabara ya ntyuka uliofikia asilimian87 ukamilike haraka kwani atasitisha mkataba kwa wakandarasi wazembe wasioweza kukamilisha miradi kwa wakati ili wananchi waweze kuitumia .
Waziri Mchengerwa amesema kiasi cha Sh1. 1 Tillion 1.1 ni fedha zilizotolewa kutekeleza miradi zinatakiwa kusimamiwa vizuri na kwa umakini mkubwa kwani miradi hiyo inatakiwa kutumika kuanzia sasa na vizazi vijavyo.
Aidha, waziri Mchengerwa ameitaka Tarura kuhakikisha jiji la Dodoma ni kipaumbele namba kwa kuweka lami kila barabara.
Post a Comment