*********
Wanariadha wa mbio za ndani na kimataifa wa mbio za masafa marefu na mafupi wameendelea kujinoa tayari kwa ajili ya michuano ya mbio za kimataifa Duniani maarufu Kilimanjaro marathon 2025 , hususani mbio za KM 21 maarufu kama YAS KILI - HALF MARATHON zinazodhaminiwa na Mtandao wa YAS kwa miaka 10 mfululizo sasa , na ikiwa ni mwaka wa 23 wa mbio hizi nchini.
" Kwakweli niipongeze kampuni ya Yas kwa kuendelea kuiheshimisha nchi yetu kwa kudhamini mbio hizi za KM 21 kwa miaka 10 sasa mfululizo , zawadi ni nzuri na sasa tupo tayari kwa mara nyingine tena kushiriki mbio hizi , Januari , 23 , 2025 "
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya YAS Kanda ya kaskazini Bw. Henry Kinabo amesema maandalizi kuelekea mashindano hayo yamekamilika na kuwatataka wananchi wakiwemo wanariadha kujitokeza kwa wingi na kufanya vizuri katika michuano hiyo huku huduma za mawasiliano chini ya udhamini wa YAS na MIXX BY YAS zikiwa zimeimarishwa kwa wageni na wafanya biashara.
Post a Comment