RAIS SAMIA AWATAKA WAHITIMU WA PROGRAMU YA MWANAMKE KIONGOZI KUWA MIFANO YA MAENDELEO KWA TAIFA

****

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wahitimu wa program ya mwanamke kiongozi awamu ya 10 na kuwataka wakawe wabunifu katika kuwa chachu ya maendeleo ya Taifa.

Rais Samia amesema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla ya miaka 10 ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) pamoja na mahafali ya kumi ya wahitimu 110 wa programu ya mwanamke kiongozi.

Pamoja na maelezo mengine, Rais ametumia jukwaa hilo kuwataka wahitimu hao kwenda kuwatengenezea njia wengine ili nao wapite na si wanawake pekee bali wanaume pia.

Aametoa angalizo la kupuuza dhana ya mila potofu kuwa mwanamke ni mtu wa nyumbani pekee na si uongozi.

"Mwaka huu ni wa uchaguzi mkuu, hivyo niwaombe wanawake mjitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi sawa na wanaume, niwaombe wote mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura ili muwe na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa". Amesema Rais Samia.

Aidha, hafla hiyo imeabatana na mkutano mkuu wa saba wa mwaka wenye lengo la kuwainua wanawake viongozi na wasichana, huku kauli mbiu ikiwa ni 'haki, usawa na uwezeshwaji'.






 

0/Post a Comment/Comments