*****
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema mwezi haujaonekana leo Ijumaa February 28,2025 na hivyo amewatangazia Waislamu wote kwamba mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza keshokutwa Jumapili March 02,2025.
Akitangaza taarifa hiyo Jijini Tanga leo, Mufti Zubeir amesema “Ndugu Waislamu leo February 28,2025 tumekusanyika sehemu zetu za Kamati ya Mwezi kwa ajili ya kuangalia mwezi wa mwandamo kwa ajili ya Mwezi wa Ramadhan lakini haijapatikana habari yoyote ya mwezi Ramadhan, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, hata wenzetu wa Kenya vilevile hawajaona mwezi mahali popote”
“Kwa maana hiyo mwezi haukuonekana,nawaelekeza Waislamu wote na kuwatangazia kwamba tunakamilisha Shaaban siku 30 na tunatarajia InshaAllah mwezi Ramadhan kuanza keshokutwa March 02,2025”
Post a Comment