.....................
Na Mwandishi wetu.
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa Ardhi na Mbunge wa jimbo la Muleba, Prof,Anna Tibaijuka, amesema ongezeko la vikundi vya waasi wanaopinga utawala wa serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Congo(DRC) ni ishara kuwa serikali hiyo imeelemewa.
Hata hivyo amependekeza kufanyika maridhiano ya amani ya kitaifa,ili kurejesha amani na utawala bora na kwamba suluhu yake ni serikali kukubali utawala kamili wa majimbo (Full Federal Republic) kama ilivyo kwa nchi ya Marekani.
Pfof. Tibaijuka,emetoa maoni hayo kwenye chapisho lake katika ukurasa wa X huku akipata mashaka dhidi ya nguvu kubwa inayoonyeshwa na kundi la waasi wa M23 kuendelea kuyatwaa baadhi ya maeneo muhimu ya nchi hiyo.
"Kazi kuu ya serikali na uhalali wake ni kulinda usalama wa raia na Mali zao,kulinda amani na sheria ukizingatia taarifa za kikundi cha M23 kuweka utawala wa serikali za mitaa na kumteua Meya wa mji wa Goma,Mukadisi Niragire Helene,pamoja na Kanali Erasto Bahati Musanga,kuwa Gavana wa jimbo kuu la Kivu Kasikazini ni ushahidi tosha kuwa serikali imeelemewa".
Aidha anasema mambo hayo yanachochewa na kushindwa kutekelezeka kwa Katiba ya nchi hiyo ya mwaka 2006 ambapo Mamlaka muhimu za serikali zilibaki Kinshasa huku ikiwa haina uwezo wa kuwahudumia wananchi wa majimbo ya mbali.
Hata hivyo Prof. Tibaijuka amewataka viongozi wa nchi za kiafrika kujisahihisha kutokana na yanayotokea nchini Congo.
Post a Comment