TMDA YAMPONGEZA RAIS SAMIA KUTWAA TUZO YA AFYA


 *****

Tausi Mbowe, Dar

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA), imempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzsnia Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa 

kutambuliwa miongoni mwa viongozi waliowezesha nchi zao kuharakisha kufikia maendeleo endelevu. 

Rais Samia Suluhu Hassan pia ametambulika katika mapambano dhidi ya vifo vya akina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. 

Rais Samia amepewa Tuzo hiyo Februari 2025 akiwa ni kiongozi na Rais Mwanamke anayeaukuma maendele kwa kasi kubwa. 

Taarifa ya TMDA ilimpongeza Rais Samia kwa uhodari wake na kutea afya za wanawake wajawazito na watoto chini ya miaka mitano jambo lililochangia kupunguza vifo kwa kiasia kikubwa. 

Mkurugenzi wa TMDA, Dk Adam Fimbo alisema Mamlaka yake ina jukumu la kulinda Afya ya Jamii na kitendo alichofanya Rais Samia ni cha kuungwa mkono kwani kinasaidia jamii kwa upande wa afya.

0/Post a Comment/Comments