*****
Waajiri na vyuo mbalimbali Tanzania vimetakiwa kutoa ushirikiano kwa Bodi ya Mikopo Nchini (HESLB), kuwafichua wadaiwa na kusimamia vizuri wanafunzi ili kupata zao ambalo litakalorudisha Mikopo baada ya kuhitimu
Wito huo umetolewa mapema leo Februari 13, 2025 jijini Dar es salaam kwenye Maaadhimisho ya miaka 20 ya Bodi hiyo na Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule ambapo amesema ili kama vyuo vitasimamia vizuri wanafunzi ambao ni wanufaika wa Mikopo basi taifa litapata wahitimu wenye tija na watakaorudisha mikopo kwa wakati na kulitumikia taifa
Aidha amewataka wahitimu wa elimu ya juu kutambua kuwa wanapohitimu kutambua kuwa wana deni walioacha hivyo kuwa waamini kwa kurejesha mikopo kwa wakati ili kuweza kuwanufaisha kizazi kijacho.
Hata hivya Dc Saad amewataka watanzania kujitokeza katika viwanja vya Biafra kinondoni kuweza kupata huduma zinazotolewa katika maaadhimisho ya miaka 20 ya HESLB.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya mashariki (HESLB) Ramadhan2 Ndongwala amesema
Katika kuadhimisha miaka 20 ya Bodi hiyo tangu kuanzishwa kwakwe 2004 inashererekea kwa kuandaa maonesho ya katika kanda tofauti hapa nchini.
Hata hivyo amesema kiwango Cha fedha kilichotolewa na serikali kimeongezeka wakati huu wa RAIS Samia Suluhu Hassan ukilinganisha na awamu zilizopota hivyo kufanya wanuafaika wengi kuweza kunuifaka na Mikopo ya elimu ya juu.
Pia amesema kuwa maonesho hayo yanafanyika katika kanda ya mashariki Dar es Salaam, Kanda ya kati Dodoma, Kanda ya Mbeya, Kanda ya Mtwara na Kanda ya Arusha, Zanzibar na Mwanza.
Post a Comment