****
Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe, Ndugu Geoffrey Kiliba, amewaonya wanasiasa ambao wameshindwa kutathmini vizuri uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesisitiza kuwa taifa haliwezi kuamini viongozi ambao wanajivunia kutaja majina ya watu au kutumia vitisho kama Wanatembea na risasi mgongoni, badala ya kutoa mifano ya uongozi bora.
Mwenyekiti Huyo amesema hayo katika Kongamano la Wanavyuo lililofanyika tarehe 15 Februari 2025 katika ukumbi wa Tanga Technical, ambalo lililenga kutoa elimu kwa vijana kuhusu umuhimu wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuwahamasisha kushiriki katika uchaguzi wa mwaka 2025.
Kiliba ameweka wazi kuwa taifa linahitaji viongozi wenye maono na mikakati madhubuti ya kuhakikisha maendeleo ya wananchi, na kwamba viongozi ambao hawana mikakati ya wazi kuhusu mustakabali wa taifa hawapaswi kuaminiwa.
Post a Comment