******
WAZIRI wa Viwanda na Biashara,Dkt Seleman Jafo ametoa siku 45 kwa shirika la Maendealeo la Taifa (NDC) kutathmini ubia wake na mradi wa ETC Cargo uliopo Mbagala Wilaya Temeke Jijini Dar es Salaam baada kubaini gawio analopata NDC haliendani na thamani halisi ya uwekezaji.
Waziri Jaffo ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anafanya Ziara ya kuangalia Mradi wa ETC ambao unamilikiwa na Ubia baina ya NDC na Kampuni ETC Cargo.
"Nimetoa maelekezo sijafurahishwa na NDC wanachokipata hapa,natoa siku 45 wakae chini baina ya mwekezaji wa hapa na menejimenti ya NDC wajadiliane na wapitie mkataba husika ili kiasi wanachotoa kiongezwe"Amesema Waziri Jaffo.
Amesema lengo la Serikali kila Mbia apate anachostahili kuzingatia uwekezaji wake.(Win win situation)
"Imani yangu kwa vile mwekezaji anamipango mikubwa ya uwekezaji na wanamipango mikubwa naimani ndani ya siku 45 watakuja na muafaka na mimi nitapata mrejesho ili watanzania wanaopata Ajira hapa waendelee kunufaika"Amesema
Aidha,Waziri Jaffo amesema ziara yake kwenye mradi wa ETC Cargo ni muendelezo wake wa kutembelea miradi inayomilikiwa na NDC ,na kubainisha kubwa amefarijika na jinsi uwekezaji mkubwa unaofanywa hapo kuzingatia watanzania wengi wamepata ajira na serikali kupata kodi yake.
Kwa upande wake,Mkurugenzi mwendeshaji wa shirika la Taifa Maendeleo NDC Dk Nicolaus Shombe,amesema mradi huo wa Ubia na NDC ni zaidi wa miaka 15 na umesaidia kuingizia serikali kodi zaidi ya Bilioni 25.
"Mradi huu umetoa Ajira za moja kwa moja kwa watanzania 139 na Vibarua 600 pamoja na Ajira za watoa huduma ,lengo letu la NDC kwa sasa ni kuhakikisha miradi yetu yote ya NDC na taasisi zingine zinalinufaisha shirika,na tumepokea maelekezo ya Waziri Jaffo tutayafanyia kazi"
Post a Comment