Na Ester Maile _ Dodoma
Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Arusha imeongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji kutoka masaa kumi na sita mwaka 2020-2021 hadi masaa 22 mwaka 2024_2025.
Ameyabainisha hayo Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hyo mhandisi Justine Rujomba leo 14 march wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya AUWSA ndani ya miaka minne.
Pamoja na uboreshaji huo mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Arusha imekamilisha miradi ya maji mikubwa kwa lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa maji safi na kuboresha huduma ya uondoaji wa maji taka katika jiji la Arusha.
Mhandisi Justine amesema z bilion 520 zimetumika katika kukamilisha miradi hiyo ya uchimbaji visima virefu ,ujenzi wa mtambo wa kutibu maji safi katika chanzo cha mto midawe pamoja na ujenzi wa ofisi za kanda na ofisi kuu kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.
Post a Comment