BEI ZA MAFUTA ZAONGEZEKA KWA MWEZI WA PILI MFULULIZO

****

Bei ya petroli kwa rejareja katika jiji la Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 6.27, dizeli kwa asilimia 6.73 na mafuta ya taa yakipanda kwa asilimia 12.02.

Kwa mujibu wa taarifa hii iliyosainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) , Dk James Andilile, imesema ongezeko hilo la bei kwa Machi linafanya petroli sasa kununuliwa kwa Sh2,996 kutoka Sh2,820, dizeli Sh2,885 kutoka Sh2,703 huku mafuta ya taa yakiongezeka zaidi.

Mafuta ya taa sasa yatauzwa Sh3,036 kwa lita moja kwa yale yaliyopitia bandari ya Dar es Salaam kutoka Sh2,710 iliyokuwapo Februari,2025.

Mafuta ya taa sasa yatauzwa Sh3,036 kwa lita moja kwa yale yaliyopitia bandari ya Dar es Salaam kutoka Sh2,710 iliyokuwapo Februari,2025.
 
0/Post a Comment/Comments