*****
Bingwa wa zamani wa masumbwi kwa uzito wa juu, George Foreman amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 76.
Taarifa iliyotolewa na familia yake na kunukuliwa na vyombo Mbali mbali vya habari duniani imesema George Foreman au maarufu kama “Big George” alifariki dunia muda mfupi uliyopita nchini Marekani.
Foreman alijulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga ngumi nzito na mapambano yake ya kihistoria, likiwamo lile la Rumble in the Jungle mwaka 1974 dhidi ya Muhammad Ali jijini Kinshasa DRC ambapo alipigwa kwa KO.
Pia, aliweka rekodi kwa kuwa bingwa wa uzani wa juu mwenye umri mkubwa zaidi (miaka 45) aliposhinda tena taji hilo mwaka 1994.
Mbali na masumbwi, Foreman alipata mafanikio makubwa kibiashara, hasa kupitia majiko yake ya umeme ya kuchoma nyama George Foreman Grill, ambapo aliuza zaidi ya majiko milioni 100 duniani kote.
Foreman ameacha familia kubwa wakiwamo watoto wake 12, wanaume watano na wote wanaitwa George wanawake saba
Post a Comment