Timu ya menejimenti ya halmashauri ya jiji la Mbeya imependekeza kugawanywa kwa jimbo la Mbeya mjini ili kuwe na majimbo mawili jimbo la Mbeya Mjini na jimbo la Uyole ambapo imesema jimbo la Mbeya Mjini litakuwa na kata 23 huku jimbo la Uyole likiwa na kata 13.
Kauli hiyo inatolewa na afisa uchaguzi wa halmashauri ya jiji la Mbeya Emmanuel Gregory kwenye kikao cha ushauri cha wilaya ya Mbeya DCC ambapo amesema hoja hiyo ilifikishwa kwenye kamati ya fedha ya halmashauri ya jiji la Mbeya na baada ya kamati hiyo kujadili iliridhia jambo hilo na kushauri miundombinu ya kata ya Mwansekwa iboreshwe.
Kwa upande wao wajumbe wa kikao cha ushauri cha wilaya ya Mbeya DCC wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na viongozi wa kimila nao wameafikiana na jambo hili.
Kikao hicho cha ushauri cha wilaya ya Mbeya DCC kimepitisha wazo hilo kuligawa jimbo la Mbeya Mjini kwa kura zote za ndio.
Post a Comment