HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA KUWA YA TAIFA


 .....................

Na Ester Maile,Dodoma

HOSPITALI ya Benjamin Mkapa iliyopo Jijini Dodoma inakusudia kuwasilisha ombi maalumu serikalini ili ipandishwe hadhi na kuwa ya taifa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kimatibabu.

Kwa kipindi cha miaka minne ya rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Hospitali hiyo imefanikiwa kupandikiza figo kwa wagongwa 25 kati ya 50, kwa kiasi cha shilingi 875 milioni ambapo kati ya hao 10 walilipiwa matibabu kupitia mfuko maalum wa Samia suluhu Hassan kiasi cha shilingi 350 milioni.

Mkurugenzi mtendaji wa Hospital  hiyo Prof.Abel Makubi, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo March 4, 2025 jijini Dodoma. 

Katika kipindi cha miaka minne serikali imeongeza huduma za kibingwa kutoka 14 hadi 20 na huduma za usingwa wa juu kutoka 7 hadi 16 kutokana na kuimalishwa kwa vifaa,wataalam na mazingira bora ya utoaji huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.


Prof.Makubi ametaja huduma hizo kuwa ni upandikizaji figo, upandikizaji  uloto,upasuaji wa mishipa ya damu, upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua pamoja na uvunjaji wa mawe kwenye mfumo wa mkojo kwa kutumia mawimbi.


Pia kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wamekuwa wakishirikiana vyema kutoa huduma na kupanua tiba za kibingwa na ubingwa wa juu wa tiba na upasuaji  kwa zaidi ya wananchi milion 14 kutoka mikoa zaidi ya 7 Tanzania.

0/Post a Comment/Comments