******
SERIKALI imesema kuwa Mageuzi ya nishati ni suala muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, hasa kwa nchi za Afrika zinazokabiliwa na changamoto za upatikanaji wa umeme ambapo Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu milioni 600 barani Afrika bado hawana umeme, hali inayokwamisha ukuaji wa viwanda na maendeleo ya jamii.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati katika Mkutano wa awali wa nishati unaowaleta pamoja maafisa wa serikali, wataalamu wa sekta, na wadau mbalimbali kujadili mageuzi ya nishati na maendeleo endelevu wa Nishati Afrika 2025 lengo likiwa ni kujadili mikakati ya kupanua upatikanaji wa nishati safi na endelevu katika bara la Afrika ambapo Serikali mbalimbali barani Afrika zinaimarisha sera na mifumo ya udhibiti ili kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi katika nishati mbadala.
Naye naibu waziri wa Nishati Judith Kapinga amefafanua kuwa Ubunifu na teknolojia vina mchango mkubwa katika kuharakisha mageuzi ya nishati barani Afrika,Mifumo mahiri ya usambazaji umeme, suluhisho za kuhifadhi nishati, na majukwaa ya kidijitali vinaimarisha ufanisi na uimara wa usambazaji wa umeme,Vilevile, ushirikiano wa kimataifa na mipango ya ufadhili inatoa msaada wa kifedha na wa kiufundi kwa miradi ya nishati safi.
Kwa upande wake Katibu mkuu Msaidizi jumuiya ya Afrika Mashariki anashughulikia miundombinu, uzalishaji, Jamii na sekta ya siasa Andrew Malueth ameeleza kuwa warsha hii inalenga kuchambua sera, fursa za uwekezaji, na suluhisho bunifu za kuboresha upatikanaji wa nishati lakini pia washirika watajadili masuala ya miundombinu, ukuaji wa uchumi, na mifumo ya udhibiti na hii itasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa na sekta binafsi ili kuharakisha matumizi ya nishati endelevu kwa maendeleo ya muda mrefu.
Post a Comment