SERIKALI YAWAONYA WATUMISHI KUGHUSHI NYARAKA ZA UHAMISHO

*****

Na,Ester...Maile,Dodoma

SERIKALI imewataka watumishi wa Umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuondoa malalamiko ya uvunjifu wa maadili,rushwa,ulevi,lugha zisizofaa pamoja na baadhi yao kughushi nyaraka za uhamisho.

Waziri wa Ofisi ya rais,Utumishi na Utawala bora ,George Simbachawene, amekemea vikali hatua hiyo na kwamba vitendo hivyo vimekuwa vikiipaka matope serikali kutokana na uzembe wa watu wachache.

Kutokana na hali hiyo,amewataka kurejea kwenye maadili ya utumishi wa umma,na kujiepusha na migogoro isiyo kuwa ya lazima kazini.

Alikuwa kwenye kikao chake na wakuu wa taasisi za Umma,kilicholenga kuwakumbusha majukumu yao na kuongeza usimamizi kwa watumishi wengine katika kutekeleza misingi ya utawala bora.

Aidha amesema jukumu la waajiri ni kuendelea kuwasimamia watumishi walio chini yao, kwa kuwapatia elimu kuhusu haki na wajibu  wao ili wanapodai haki wajue kuwa wanapaswa pia kutimiza wajibu wao.

Vile vile katika mwaka wa fedha 2024/25 serikali inatarajia kupandisha vyeo watumishi 219042 na kubadilisha kada watumishi 6910.


          


 

0/Post a Comment/Comments