TANTRADE KUKARABATI UWANJA WA MAONYESHO YA BIASHARA

...,.,.......,.,...

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE) imesema kuwa katika  kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita mifumo ya taarifa za biashara na masoko imeboreshwa .

Akibainisha hayo leo Machi 13, 2025 jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo  Latifa Khamis amezungumza  na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne chini ya Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Rais Samia amesisitiza sana matumizi ya mifumo serikalini ili kuhakikisha wananchi  wanapata huduma kwa wakati.

Katika hatua nyingine Latifa ameongeza kuwa mpango wa baadaye katika kujenga uwezo wa Taasisi na kujiendesha kwa ufanisi yatafanyika maboresho  katika uwanja wa maonyesho wa Mwl.Julius Kambslage Nyerere ambao utaboreshwa na kuwa wa kisasa ili kuendana na viwango vya kimataifa.

Pia Latifa amesema kwa Tanzania tuna bidhaa zenye fursa katika biashara amabazo ni korosho,  na  parachichi.

Vilevile washiriki waongezeka kutoka 2925 hadi kudikia 300 ambapo nchi 28 za ongezeka katika kukuza ukuzaji wa soko.


 

0/Post a Comment/Comments