TBS YATENGA ZAIDI YA SH.MILLION 350 KILA MWAKA


****

Shirika la viwango Tanzania limejiwekeq utaratibu wa kutenga zaidi ya milioni 350 kila mwaka kwa madhumuni ya kuhudumia wajasiliamali wadogo bila ya malipo yoyote 

Ameyaeleza hayo Mkurugenzi mtendaji wa shirika la viwango Tanzania Dkt Ashura Katinzi wakati akizungumza na waandishi wa habari leo 18march 2025 ,akieleza mafanikio ya shirika hilo kwa kipindi cha miaka minne.

Pia leseni wanazopata wajasilimali wadogo zimewasaidia wazalishaji kuzalisha bidhaa bora na kuzifanya bidhaa hizo kuweza kuaminika sokoni na kufanya biashara nje ya mipaka ya Tanzania.

Vile vile katika kuimalisha ukaguzi wa bidhaa zinazoingia nchini kutoka nchi za nje Shirika la viwango Tanzania linahakiki bora wa bidhaa na magari yanayotumika kabla ya kusafirishwa kuja nchini.

Hata hivyo jumla ya shehena za bidhaa 18588 zimekaguliwa sanjari na magari 162160 bidhaa hizi zianakaguliwa kwa lengo la kuiepusha Tanzania kuwa jalala la bidhaa duni pamoja na kulinda afya ,usalama na mazingira ya watumiaji.



0/Post a Comment/Comments