Na Ester Maile..Dodoma
Benki ya maendeleo imewekeza shilingi bilion 250.7 katika ukuaji uchumi na ajira ikihusisha sekta za utalii ,viwanda na usafirishaji.
Haya yameelezwa leo march 20.2025 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya maendeleo Lilian Mbassy wakati akieleza mafanikio ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha shilingi bilion 24.7 zimewekezwa katika kuboresha miji ma makazi ambapo shilingi 11.5 zimewekezwa katika nishati safi na nafuu katika miradi na upanuzi wa Nishati ya umeme vijijini.
Mbassy amesema TIB ni taasisi ya kisera amabayo ina majukumu ya kutekeleza sera na mikakati ya kitaifa hususani kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Vile vile Benki ya maendeleo TIB itaendelea kushirikiana na SHIRIKA LA UMOJA WA KIMATAIFA LA MAENDELEO YA VIWANDA(UNIDO) katika kuchochea matumizi ethanol kama chanzo mbadala cha nishati safi na nafuu ya kupikia kupitia mradi wa "waste to energy".
Pia benki ya maendeleo imejipanga kushirikiana na taasisi za fedha za kimataifa ili kupata mikopo ya riba nafuukwa ajili ya kuhifadhili miradi yenye Athari chanya kwa jamii na uchumi.
Post a Comment