Na Tausi Mbowe
Huduma za afya ni jambo la msingi ambalo linatakiwa kusimamiwa na Serikali ili kuhakikisha afya za wananchi wake zinakuwa bora.
Katika kuhakikisha hilo linafanyika kwa weledi mkuu Serikali kupitia taasisi zake ikiwamo ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imekuwa ikisimamia misingi imara kwa maslahi ya Taifa.
Leo Jumatano, Machi, 2025 Rais Samia Suluhu Hassan ametimiza miaka minne tangu aingie madarakani baada ya mtangulizi wake Rais John Magufuri kufariki dunia akiwa madarakani.
Tangu alipoingia madarakani, mwanamama huyo shupavu ameuthibitishia ulimwengu kuwa anaweza kuongoza vyema kwa kuzingatia demokrasia, haki na utu wa wanachi haichezewi.
Aidha, Dkt Samia katika kipindi chake cha uongozi amehakikisha sekta ya Afya inaboreshwa na wananchi wanapata huduma bora ili kupunguza vifo katika Taifa.
Katika kipindi hicho cha uongozi wake, TMDA imefanikisha mambo 12 ikiwa ni pamoja na kusajiliwa viwanda 18 vya dawa, 140 vya vifaa tiba na Vitendanishi hivyo kuchangia katika uwekezaji.
Vileviile TMDA katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia imesajili zaidi ya bidhaa 8303 za dawa na 3,019 za Vifaa Tiba na Vitendanishi baada ya kujiriddhisha na ubora na ufanisi wake.
Jambo lingine ni kuongeza bajeti kulilowezesha utoaji wa huduma kwa ufanisi na kutoa gawio la Sh23. 3 bilioni kwa Serikali.
Lingine ni uwekezaji wa Sh15 bilioni katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya maabara ili kuwezesha kufanya maamuzi ya kisayansi.
Pia matumizi ya mifumo ya kielotrinic katika huduma za utoaji vibali jambo lililowesha kutolewa kwa saa 24.
Mamlaka hiyo pia imeendelea kushikiria cheti cha Ithibati na Ithibati ya Maabara kwa kiwango cha ISO katika utoaji wa huduma bora.
Sambamba na hilo Mamlaka hiyo pia imewezesha asilimia 98 ya bidhaa kukidhi ubora na ufanisi hivyo kuhakikusha usalama wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika soko.
Mamlaka hiyo pia imeongeza maabara hamishika mara dufu kutoka 19 hadi kufikia 28 ili kuimarisha zoezi la uchunguzi wa sampuli.
Kwa miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita pia mamlaka hiyo imekamilisha ujenzi wa miundombinu ya tanuri la kuteketeza zisizofaa lililopoa eneo la Nala jijino Dodoma ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia katika soko ni zile tu zenye ubora, ufanisi na usalama.
Pia mamlaka hiyo imeongeza wafanyakazi kutoka 278 hadi kufikia 421 hivyo kuongeza fursa ya ajira nchini.
Jambo lingine ni ongezeko la vituo vya ufuatiliaji wa mahudhu ya dawa pamoja na upanuzi wa ofisi kwa kuongeza sakafu tatu kwenye jengo la ofisi ya Makao Makuu Dodoma.
Post a Comment