WANAWAKE TUADHIMISHE SIKU YETU KWA KUJIPAMBANUA, KUJIONGEZA NA KUWEKEZA - BALOZI LIBERATA MULAMULA (MB)


       ******

WAKATI wanawake wakiadhimisha siku yao, Machi 8 mwaka huu, Mh. Mbunge Balozi Liberata Mulamula amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa wote katika kutambua nafasi na mchango mkubwa wa mwanamke katika jamii, uongozi kwa mustakabali mzima wa Taifa na dunia.

Akizungumza leo, amesema "Kama alivyosema Mhe. Waziri Dorothy Gwajima Maadhimisho ya mwaka huu 2025 ni ya kipekee kwa kuwa yanaambatana na miaka 30 ya utekelezaji wa Azimio la ulingo wa Beijing (1995). Hivyo inatupa fursa kutathimini tulikotoka tangu kupitishwa Maazimio ya Beijing,

"Tulipofikia katika utekelezaji wa Maazimio hayo na tuendako. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji.” Lengo likiwa ni kuhamasisha jamii kukuza Usawa, Haki na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana. Tuendelee kuunga mkono juhudi za Serikali na wadau kuhusu Usawa wa Kijinsia nchini," alisema.

 Aliwashauri wanawake kukusonga mbele kwa vitendo hususan kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu, wanawake wajipambanua, wajiongeza, wapambane, wawekeza, wajiamini na wajitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

0/Post a Comment/Comments