..................
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara Stephen Wasira amesema chama hicho hakina mpango wa kuiachia serikali chama kingine kwa sababu wakati wanafanya harakati za ukombozi na kutafuta uhuru hawakukubalina na yeyote kwamba wataondoka baada ya kipindi fulani.
Wasira ameeleza hayo baada ya kuwasili katika ofisi za chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Mbeya. Na kupata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa chama wanachama, machifu pamoja na wananchi wa Jiji la Mbeya.
Wasira atarajiwa kufanya ziara ya siku nne Jijini hapa.
Post a Comment