......................
Taasisi ya Wakala wa Vipimo imefanya uhakiki wa vipimo 392652 kati ya hivo vipimo 102969 vilikutwa na mapungufu ambayo yalirekebishwa na kuruhusiwa kuendelea kutumika na vipimo 5607 vilikataliwa kutumika baada ya kuonekana na mapungufu hayawezi kurekebishika.
Afisa Mtendaji Mkuu wakala wa Vipimo (WMA) Albon Kihulla ameeleza hayo
wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari akizungumzia mafanikio ya Taasisi hiyo leo 25,march 2025, jijini Dodoma.
Pia Wakala wa Vipimo imechangia shilingi bilioni 7 kwenye mfuko mkuu wa serikali kufikia February 2025 wakala imekwisha changia kiasi cha bilion 3.8.
Aidha wakala inapima matenki ya malori 60 kwa siku ongezeko la idadi ya matenki ya liyo hakikiwa imepelekea kurahisisha kiasi kikubwa cha mafuta kuondoka kwenye maghala na kiasi cha mafuta yanayosafirishwa kuenda nje ya nchi na mikoa mbalimbali kuondoka kwa haraka kwa kuwa magari yanatumia muda mfupi katika uhakika wake.
Vile vile Wakala wa Vipimo inaendelea kutoa huduma za uhakika wa kiasi cha mafuta (Jamii ya petroli na mafuta ya kula ) yanayoingia nchini kupitia bandari za Dar es Salam, Tanga na Mtwara na lita 30645930571 za mafuta kwa meli 546 zikizowasili nchini kukiwa na ongezeko la meli 136 mwaka 2021 _2022 hadi meli 174 hadi kufikia Februari 2025 meli zimeongezeka kutokana na maboresho yaliyofanywa na serikali katika utoaji wa huduma na miundombinu ya bandari.
Post a Comment