Mkutano Mkuu wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) umefanyika Aprili 28, 2025,
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa chama na kupitisha wagombea
wa urais wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Katika mkutano huo, Majaliwa Kyara amechaguliwa kuwa mgombea urais wa
chama hicho kwa upande wa Tanzania Bara.
Akihutubia wajumbe wa mkutano huo, Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty
Nyahoza, amesema kuwa mageuzi ya uchaguzi yaliyofanyika nchini Tanzania
yamezingatia viwango vya kimataifa na si matakwa binafsi ya watu.
Nyahoza amesisitiza kuwa demokrasia inahusisha kuheshimu kanuni zilizokubalika
kimataifa, akifananisha hali hiyo na michezo ambapo viwango vya kimataifa
huamua ubora wa maamuzi badala ya hisia za washiriki.
Aidha, amesema Tanzania inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari na maoni ya
wananchi, jambo linalothibitisha ustawi wa demokrasia nchini.
Post a Comment