CHANGAMOTO YA UPUNGUFU WA WATUMISHI KUTATULIWA - SIMBACHAWENE



...........................

 NA Ester Maile...Dodoma 

Serikali kupitia Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora imetafuta namna bora ya kuondoa changamoto ya upungufu wa watumishi katika maeneo mengi .

Hayo yameelezwa leo 17,march 2025 na Waziri wa Nchi ,ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora George Simbachawene  wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma akiongelea mafanikio ya wizara katika kipindi cha miaka minne .

Hata hivyo ofisi ya rais  imejenga mfumo wa Tathmini ya mahitaji ya Rasilimawatu (HR Assessment) mfumo huo wa Tathimini ya mahitaji ya Raslimaliwatu ni msaada mkubwa kwanj unabainisha idadi ya watumishi walioko katika kila kituo cha kazi na upungufu au zaidi iliyopo ili kazi kuwa na idadi ya watumishi sahihi katika sehemu za utekelezaji wa majukumu yao.

Vilevile kupitia mfumo huo Taasisi  za umma zimewezesha kuondoa mahitaji ya watumishi hadi kufikia men 2024 mfumo umechakata takwimu kwa mikoa yote 26 ya Tanzania na kuzifikia taasisi  534.Baada ya majumuisho ya taasisi za tathmini ya mahitaji ya watumishi kwa taasisi hizo ilibainika kuwa  watumishi  waliopo ni 597396 mahitaji1036762 na kupelekea  upingufu wa 441366 ambayo ni zaidi ya asilimia 73 ya watumishi waliopo.




 

0/Post a Comment/Comments