DK MPANGO KUTOA TUZO YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU

****
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Philip Mpango, kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, itakayofanyika Aprili 13, 2025.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Aprili 7, 2025, jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa hafla hiyo inalenga kutambua na kuenzi mchango wa waandishi bunifu katika kukuza lugha, utamaduni, na fikra za maendeleo nchini

Tuzo hii, iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni ishara ya kumuenzi kutokana na mchango wake mkubwa katika Uandishi Bunifu.

“Mwalimu Nyerere alikuwa mwandishi wa mashairi na pia alifanya kazi ya kutafsiri vitabu vya mwandishi nguli William Shakespeare. “ amesema Mkenda

Lengo kuu la tuzo hizi ni kuhamasisha kizazi kipya cha waandishi bunifu na kuthamini wale wanaoonyesha ubunifu wa hali ya juu na mchango mkubwa kwa jamii.

















 

0/Post a Comment/Comments