BILION 20 ZA WEKEZWA KATIKA KIWANDA CHA WANGA NA GLUKOSI


:::::::

Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara imewekeza bilion ishirini katika kiwanda cha uzalishaji wanga na glukosi ya maji huko mkoani mbeya.

Haya yameelezwa leo 15 may 2025 jijini Dodoma na waziri wa viwanda na biashara Seleman Jaffo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kueleza mafanikio ya wazara hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita

Jaffo amesema kiwanda pekee hapa Tanzania kinachozalisha wanga na glukosi kilichopo mkoani mbeya kinazalisha glukosi ambayo inatoa bidhaa za viwandani ikiwemo biskuti,ice cream pipi na madawa.

Pia kiwanda kinauwezo wa kuzalisha tani 15000 za wanga na tani 12000 za glukosi ya maji kwa mwaka kutokana na mahitaji tani 40000hadi tqni 45000 hadi kufikia mach 2025 kiwanda kimezalisha tani 187 za wanga na tani 700 za glukosi ya maji .

Aidhakiwanda kimetoa ajira themanii za wafanyakazi wa moja kwa moja na ajira ishirini za mda mfupi.


 

0/Post a Comment/Comments