Serikali kupitia wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi imefanikiwa kuanzisha chombo cha kusimamia madalali ili kuepuka migogoro kwa wananchi .
Haya yameelezwa na waziri wa Ardhi nyumba maendeleo ya makazi Deogratious Ndejembi wakati wakizungumza na waandishi wahabari leo 23 mei 2025 jijini Dodoma akieleza mafanikio ya sekta hiyo kwa kipindi cha miaka minne.
Pia Ndejembi amesema serikali ipo katika mchakato wa kutunga Sheria ya milking ambayo itaanzisha Mamlaka ya usimamizi wa sekta ya Milki (real estate regulatory authority)ambayo itakuwa na jukumu la kuunda mfumo madhubuti wa usimsmizi wa sekta hiyo.
Vilevile mfumo utasaidia kutoa taarifa sahihi za wadau wa soko la milki na kuongeza ufanisi wa wasau wa sekta hyo ili kuepusha wananchi kuendelea kudhurumiwa ardhi zao.
Post a Comment