Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Suleiman Jaffo, wakati wa maonesho ya kibiashara yaliyoandaliwa na Equity Bank Tanzania, Mkuu wa Chuo cha CBE, Profesa Tandi Luoga amesema fursa zilizopo katika sekta ya utalii hazipaswi kupuuzwa,amesisitiza kuwa kutumia vyema urithi wa asili na tamaduni za taifa kunaweza kuifanya Tanzania kuwa kivutio kikuu cha utalii na eneo lenye fursa pana za uwekezaji katika malazi, usafiri na huduma za kijamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Equity Bank Tanzania, Isabela Maganga amesema mkutano huo umeleta pamoja wawekezaji na wafanyabiashara kutoka zaidi ya nchi 15, huku wajumbe zaidi ya 230 kutoka Afrika, Ulaya, Asia na Mashariki ya Kati wakijisajili kushiriki,na amesema benki yao iko tayari kuunga mkono safari ya uwekezaji nchini kwa kuunganisha wadau, kuwezesha mitaji, na kuinua biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana, ikiwa ni sehemu ya kuchochea ukuaji wa uchumi jumuia.
Post a Comment