Abou Lyiongo, Ahmed Kipozi kakosekana hapo Jlius Nyaisanga, Majura na Mzee Tido Mhando japo Tido nafikiri alikuwa mkubwa kwao sana na Abou alikuwa mdogo wao.
Wote walianzia RTD kisha wote kwa nyakati tofauti walienda nje watatu BBC, Tido, Charlesna Majura yy aliripoti kutokea Dar.
Kipozi yy alienda kati ya China au Japan na Lyiongo Ujerumani.
Kisha wote walirejea Tz.
Nyaisanga na Chaz wakanzisha Radio One baadaye wakamuita Majura.
Lyiongo na Kipozi wao walianzisha Radio Uhuru 2000 nami nikiwa natoka tu chuo mwaka 1999 baadaye mwaka 2000 nikajiunga nao pale CCM Lumumba jengo la mkoa ghorofa ya nane. Nilifanya nao kazi hawa wazeee ni mentor wazri sana wanajua kufundisha kwa vitendo uandishi.
Tido yy aliendelea kusalia BBC kwa muda mrefu mpaka pale alipostaafu na kuitwa na Rasi Kikwete aje aongoze TBC..
Chaz yy alipotoka Radio one ndiyp akaenda BBC akakaaa huko mpaka alipostaafu ndiyo akarudi nchini kwa kuitwa na rafikiye Tido kuja kuongeza nguvu Azam wakati huo Tido alipotoka TBC akaenda Azam.
Mungu ampuumzishe Uncle Charles .. Ametuachia funzo kubwa sana.
Aikuwa Mtu Raimu sana
Post a Comment