******
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafugwa, amekabidhi magari matano aina ya Toyota Land Cruiser kwa wakuu wa polisi wa wilaya za Kwimba, Magu, Misungwi, Ilemela, na Nyamagana.
Magari hayo yametolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camillus Wambura, ikiwa ni sehemu ya juhudi zinazoendelea za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha miundombinu mbalimbali ya Jeshi la Polisi na kuongeza ufanisi wa kazi.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Kamanda Mutafugwa alitoa shukrani kwa IGP Wambura kwa namna ambavyo anaendelea kushughulikia changamoto za kiutendaji ndani ya Jeshi hilo, na kusisitiza kuwa magari hayo yatasaidia kuongeza ufanisi wa kazi hasa katika shughuli za doria na ulinzi wa raia na mali zao.
Kwa niaba ya wakuu wa polisi waliopokea magari hayo, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ilemela alitoa shukrani kwa uongozi wa Jeshi la Polisi na kuahidi kuyatunza magari hayo pamoja na kuhakikisha yanatumika ipasavyo katika kudumisha amani na usalama katika maeneo yao ya kazi.
Post a Comment