MADINI AINA YA ALMAS YA SH, BILIONI 1.7 YAKAMATWA MWANZA .


                :::::::

Almas yenye Thamani zaidi ya bilioni 1.7 imekamatwa ikisafirishwa kinyume na utaratibu katika uwanja wa ndege wa mwanza. 

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari waziri wa madini Antoni Mavunde katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema madini hayo yamekamatwa Mei 18 Mwaka huu yakisafirishwa na raia wa kigeni yakiwa kwenye mabegi manne

Aidha Waziri Mavunde amesema serikali imesikitishwa na kitendo hicho cha utoroshwaji wa madini hayo na inalaani vikali vitendo vya namna hiyo 

Sambasamba na hayo mavunde amesema kwa mwaka wa fedha 2015 /2016 serikali ilikusanya billion 162 kutokana na biashara ya madini lakini kutokana na udhibiti mkubwa wa utoroshaji wa madini mwaka wa fedha 2024 /2025 mpaka mwezi mei serikali imekusanya shilingi billion 925 huku lengo ikiwa ni kufikisha tirion moja .

 




0/Post a Comment/Comments