BENKI ya NMB imesema itapeleka vitanda na mashuka na baadhi ya vifaa vya shule katika Shule ya Sekondari Pugu jumla vyenye thamani ya Sh milioni 10.
Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Alfred Shayo amesema hayo katika maadhimisho ya mbio za hisani za Pugu Marathon zilizofanyika maeneo ya Sekondari ya Pugu, Dar es Salaam leo.
Amesema fedha zilizopatikana kwa ushiriki wa watu 6,000 katika mbio hizo, zitasaidia ununuzi wa vitabu, na vifaa tiba.
“Hatua hii sio tu kurudisha kwa jamii, bali pia kuimarisha afya, lakini ushiriki wa watu wengi ndio utafanikisha malengo haya,” amesema Shayo.
Katika hatua nyingine, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu ametaja malengo ya kuanzishwa kwa mbio hizo kuwa licha ya kujenga afya, lakini pia kuendeleza kituo cha Hija cha Pugu.
Amezungumzia ujenzi wa vituo 14 njia ya misalaba ambapo hadi kukamilika kwake vitagharimu Sh milioni 546, kuwa ni miongoni mwa malengo ya mbio hizo.
“Pia kujenga jengo la utawala Sh milioni 200 inajumuisha baadhi ya vitendea kazi na ufundi hata hivyo ujenzi umeenza,” amesema Askofu Mchamungu.
Ukosefu wa fedha na miradi hiyo kushindwa kukamilika kwa wakati ameitaja kuwa ni moja ga changamoto walizonazo. Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo wadhamini kuangalia namna ya kusaidia suala hilo.
Aidha, amesema wataendelea kusimamia lengo la mbio hizo kwa kufanya matendo ya huruma ikiwemo kurudisha kwa jamii.
Awali akisoma risala kuhusu mbio hizo, Makamu Mwenyekiti wa Maandalizi Pugu Marathon, Yalanda Kahunduka alisema kwa miaka miwili iliyopita wamefanikiwa kushirikisha watu 10,000, sambamba na kutangaza chapa ya Pugu.
Hatua ya ushirikishaji wa idadi hiyo imefanikisha kununua mashuka na vifaa vya milioni 2 katika hospitali ya Rugambwa iliyopo, lakini pia vifaa vya Sh milioni 3 Hospitali ya Pugu zote zilizopo Dar es Salaam.
Pia wamefanikiwa kukarabati nyumba vya Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimuu Julius Nyerere aliyokuwa akiishi.
Post a Comment