RAIS DKT, SAMIA AMPONGEZA BALOZI MULAMULA(MB), KUWA MJUMBE MAALUM WA WANAWAKE AU

:::::

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan amemshukuru na kumpongeza Waziri Mstaafu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mbunge Balozi Liberata Mulamula, kwa kuteuliwa kuwa mjumbe maalumu wanawake katika Umoja wa Nchi za Afrika (AU).

Rais Dk.Samia ametoa pongezi hizo, leo, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizindua Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001(Toleo la Mwaka 2024), uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC) na kuudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Mbunge huyo Balozi Mulamula.

"Lakini katika eneo lingine, Mheshimiwa Liberata Mulamula na yeye juzi juzi tu hapa, amepata nafasi ya kuwa mjumbe maalumu wa AU, katika mambo ya wanawake Barani Afrika tunakushukuru sana," alisema.

Alisema Tanzania imeendelea kuweka heshima kubwa kimataifa kupitia viongozi wake ambao wameendelea kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi duniani, akiwemo Rais 

Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Nchi za Kusini mwa Afrika, (SADC),Spika wa Bunge Dkt.Tulia Ackson ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU) , Profesa Mohamed Janab ambaye amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya (WHO) Kanda ya Afrika na wengineo.


 

0/Post a Comment/Comments