RC MWANZA AZINDUA JARIDA LA KUKABILIANA NA GUGUMAJI ZIWA VICTORIA

          ::::::::

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ameigiza bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria kuhakikisha Jarida waliloliandaa kuhusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji jipya katika ziwa victoria (Salvinia Molesta) linawekwa katika mifumo mbalimbali ili jamii iweze kuona, kusoma na kusikiliza vizuri.

Mtanda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa jarida hilo linalohusu kukabiliana na uvamizi wa Gugumaji katika Ziwa Victoria ambapo amesisitiza umuhimu wa kuliweka katika mifumo mbalimbali ikiwemo mfumo wa nakala na mitandaoni ili wananchi wengi waweze kupata nafasi ya kulisoma na kupata uelewa.

Nae Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Dkt. Renatus James amesema Jarida hilo ni maalumu na limelenga kuhakikisha taarifa muhimu ya shughuli mbalimbali na jitihada ambazo zimefanywa na Serikali katika kupambana na Gugumaji ikiwemo mipango ya baadae

Zoezi hilo la uzinduzi wa Jarida la bodi ya maji bonde la ziwa Victoria limeshuhudiwa na viongozi mbali mbali Pamoja na wafanyakazi wa bonde la ziwa viktoria mkoani mwanza.




 






0/Post a Comment/Comments