Serikali Imesema inamatarajio ya kuwa na kadi moja itakayomwezesha mwananchi kuitumia katika mahitaji mbalimbali ikiwemo viwanja vya michezo, kivuko cha Kigamboni, pamoja na stendi ya mabasi ya Magufuli Bus Terminal huku Lengo kuu likiwa ni kuifanya N-Card kuwa suluhisho la kidigitali linalogusa maisha ya kila Mtanzania.
Serikali pia inalenga kuhakikisha kadi hiyo inatumika kwenye usafiri wa mabasi yaendayo haraka (DART) na huduma nyingine nyingi kulingana na mahitaji ya jamii.
Hatua hii imejidhihirisha leo Mei 15, 2025, baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb), kutembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC) kilichopo Kijitonyama, Dar es Salaam, ili kujionea namna Mfumo wa N-Card unavyofanya kazi.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alipokelewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa pamoja na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mkurugenzi Mkuu wa UDRT Waziri Kindamba na Mtendaji Mkuu wa DART Dkt. Athuman Kihamia.
Waziri Silaa, alisisitiza kuwa ujio wa N-Card ni hatua muhimu katika kutekeleza azma ya Serikali ya kuhakikisha teknolojia inakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi.
Alisema, “N-Card ni mfano mzuri wa jinsi Serikali inavyoweza kutumia TEHAMA kuboresha huduma za umma, na tunatarajia mfumo huu utasaidia katika kuondoa vikwazo vilivyokuwepo awali.”
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa Akizungumza na Waandishi wa habari mapema Leo mara Baada ya ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (Mb), akiaga mara baada ya kutembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Data Kimtandao (NIDC) kilichopo Kijitonyama, Dar es Salaam,
Post a Comment